KURUNZI YA AFRIKA

Ubrica ni shirika ambalo linahusika na kuboresha Sayansi ya vyote vilivyo hai pamoja na afya ya kila mwananchi.
Wazo la kufanya haya lilitokana na kuzoroteka kwa hali ya afya barani Afrika ambako kumesababishwa na ukosefu wa fedha za kulipia matibabu. Pia, hospitali hazina fedha za kutosha za kununua vifaa bora vya kutekeleza matibabu.

Ubrica ni ufupisho wa jina halisi ambalo ni “Ustawi Biomedical Research Innovation and Industrial Centers of Africa”. Neno Ustawi pia ni ufupisho kumaanisha “US to Africa wealth initiative” (mpango wa kuboresha utajiri kutoka Marekani hadi Afrika).

Ubrica imegawanywa katika matawi matatu makuu ambayo ni:
-Mkataba wa tarakimu au kwa jina maarufu “Smart contract”
-Ushiriki wa binadamu au “Human engagement”
-Miradi au “Projects”

Mkataba wa tarakimu
Hii ni itifaki ya tarakilishi ambayo jukumu lake ni kuwezesha, kudhibitisha na kutekeleza mapatano ya kuaminika. Kupitia mkataba wa tarakimu, kubadili fedha, mali au vitu vya thamani kunawezekana kwa njia rahisi yenye uwazi na isiyo na mvutano. Mfumo uo huo ndio utakao tumika katika soko yetu ya mtandao: Soko Janja (mengi zaidi yatajadiliwa kwenye tawi la ushiriki wa binadamu). Naam, mchumia juani hulia kivulini. Kwa kuzingatia msemo huu, Ubrica itaanzisha mfumo wa kutuza wafanyao kazi yao kwa bidii na kwa njia ifaayo. Hatimaye mbinu hii itahakikisha kuwa wateja wanapokea bidhaa na huduma bora zaidi. Muuzaji atatuzwa kulingana na alama ambazo atakusanya kutoka kwa mnunuzi katika mfumo wa tarakimu ambao utaweza kutumika na kila mmoja baada ya kupokea bidhaa ama huduma.

Kupitia mfumo huu, Ubrica imeunda sarafu za kidijitali zijulikanazo kama Ubricoin. Sarafu hizi ndizo zitakazo husika na kumzawadi yeyote ambaye atatekeleza majukumu yake kwa bidii, uwazi na ustadi. Pia zitatumika kuendeleza ufahamu kuhusu umuhimu wa kuishi vyema, lishe bora na kutembelea zahanati au hospitali ili kugundua magonjwa mapema. Utumiapo sarafu hizi, sehemu ndogo huwekezwa katika health fund ili uwapo muwele utapata matibabu kwa bei nafuu.
Ubricoin moja ni shilingi hamsini. Kwa sasa, wananchi wanapokezwa Ubricoin elfu kumi kila mmoja ili kuhakikisha kila mwananchi ameshikilia sarafu zake katika mfuko wake wa kidijitali. Kupitia njia hii, thamani yake itadizika kulingana na idadi ya watu walio na sarafu yenyewe kwenye mfuko wao au jinsi wanavyoitumia. Yaani v=n2, ambapo v inasimamia value na n inasimamia number (sheria ya Metcalfe).
Hakika kizuri chajiuza! Kufikia sasa, sifa za sarafu hizi zimesheheni na kusambaa toka bara la Afrika hadi nchi za Uingereza na Marekani.

Ushiriki wa binadamu
Tawi hili linahusika na jinsi ambavyo Ubrica imeweka mikakati itakayo boresha hali ya kifedha ya wananchi. Mikakati hii inahusisha uuzaji wa bidhaa kupitia soko la mtandaoni linalojulikana kama Soko Janja.
Wazo la kuanzisha soko hili lilitokana na ujuzi kuwa bidhaa za wakenya hazipati soko la kutosha kukimu mahitaji ya wauzaji. Kwa mfano, mkulima anayejihusisha na uuzaji wa mimea na mifugo huwa na wakati mgumu kupata faida kwa kazi zake kwa sababu mimea mingi huwa imeagizwa kutoka nchi za nje. Hivi basi inakuwa wazi kuwa mkulima huyu anachanika kwenye mpini na kufa njaa. Jambo hili linasikitisha hususan wakati ambapo ataugua kwa sababu fedha zake zimeadimika kama maziwa ya kuku, basi hataweza kujilipia matibabu. Kando na hayo, hali yake ya kimaisha itazidi kudidimia.
Kupitia Soko janja, mkulima huyu ataweza kupanua mipaka yake ya kupata soko na kuuza bidhaa zake kisha kupata fedha maridhawa.
Ili kutangaziwa bidhaa zako mle, unapiga picha kisha unazifafanua kwa lugha itakayomvutia mnunuzi na pia bei yazo, bila kulipishwi chochote.

Miradi
Mbuga za Sayansi na teknolojia kwenye vyuo vikuu (USTPs)
Zitajengwa sitini na sita karibu na kila chuo kikuu Kenya. Lengo la mbuga hizi ni kuwa vituo vya kufanyia utafiti na kuzitafutia soko bidhaa ambazo zitaundwa kutokana na utafiti ule. Wanafunzi wa vyuo hivi ndio watafanya kazi mle, pamoja na wataalamu ambao wana ujuzi katika nyanja mbalimbali za utafiti. Mbuga hizi zitawapa wanafunzi nafasi ya ajira ya mapema badala ya kumaliza shule na kujihusisha na maovu au kutafuta kazi na kuambulia patupu.

Vituo vya Ubrica vya soko la rejareja na klinikii (URCCs)
Hivi ni vituo vya biashara na uboreshaji wa afya ambavyo vitakuwa na msingi wao vijijini. Kutakuwa na vitengo viwili katika kila kata na wilaya kubwa zikiwa na nyingi kidogo. Idadi ya vitengo imewekwa kuwa 100.
Vituo hivi vitakuwa na:
⦁ Karakana.
⦁ Vituo vya soko rejareja.
⦁ Vituo vya kliniki.

Karakana
Haya ni maeneo ambayo yatahusika na kuboresha hali ya mazao na kuongeza thamani kwa bidhaa zilizozalishwa nchini. Kutakuwa na vipengele vya usindikaji wa mimea na bidhaa na sehemu za kuunda bidhaa mpya kati ya mengine kwa ajili ya kuboresha vinavyoonekana. Hatimaye, hii itahakikisha uhifadhi wa bidhaa za chakula na mimea ambazo lazima kuhifadhiwa mahali safi ili kuzuia magonjwa.

Vituo vya soko rejareja
Hivi ni vituo vya kuonyesha bidhaa kutoka kwenye karakana ili kuvutia wanunuzi. Bidhaa zenyewe hupelekwa hapa ili wanunuzi waweza kuzipata kwa urahisi. Pia, picha za bidhaa hizi zinaweza kuchukuliwa na kuwekwa kwenye duka la rejareja la mtandaoni linalojulikana kama Soko Janja ili kuvutia wanunuzi zaidi.

Vituo vya kliniki
Kutokana na kukusanya fedha maridhawa baada ya kuuza bidhaa, watu wataweza kulipia huduma zao za matibabu. Vituo hivi vya kliniki vitawapa watu huduma bora za afya. Wagonjwa walio na Ubricoin wataweza kupokea huduma hii kwa bei nafuu kwa magonjwa yoyote yale. Huduma hii itahakikisha kuboreka kwa viwango vya maisha na hatimaye kukuza taifa lenye afya.

Kwa maelezo zaidi, waweza kutembelea tovuti zetu katika:
https://ubricoin.ubrica.com/white-paper/
http://sokojanja.com/
http://uwc.ubrica.com/
https://ubricoin.ubrica.com/

Mwandishi, Barbara Kimani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *